Monday, 4 June 2018

Sugu Kuja na Wimbo Mpya Atakaoupa Namba yake ya Gerezani

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) ambaye pia ni msanii nguli na mkongwe kwenye game ya hip hop ya bongo, anatarajia kuachia kazi yake mpya hivi karibuni aliyoipa jina la namba yake ya jela, 219.

Sugu anaachia wimbo huo ikiwa zimepita siku 25 tangu alipotoka gerezani kwa msamaha wa Rais John Magufuli, Mei 10, 2018, na kusema kwamba wimbo huo utabeba mambo mbali mbali aliyokutana nayo akiwa jela kama mfungwa.

“Maandalizi na kila kitu kipo poa na soon nitautoa wimbo wangu nilioupa jina la 219, nimeimba mimi mwenyewe na nimezungumzia hali ya nchi, experience yangu niliyoipata gerezani na mambo mengine, ni ngoma nzuri kabisa”, amesema Sugu.

Sugu amesema ameamua kuita jina hilo la namba yake ya ufungwa kwa sababu ni namba inayojulikana nchi nzima.

No comments:

Post a Comment