Saturday, 9 June 2018

Simba SC Tutakufa na Kupona Kupata Matokeo Kwenda England - Djuma


Kuelekea mechi ya fainali ya SportPesa Super kesho mjini Nakuru, Kenya kati ya Gor Mahia FC dhidi ya mabingwa wa mpira Tanzania Msimu Huu Simba SC, Kocha Masoud Djuma amesema watakufa na kupona kupata matokeo.

Mrundi huyo aliyechukua nafasi ya Mfaransa Pierre Lechantre aliyeisusia timu kufuatia kuomba mkataba mpya, amesema hakuna ambaye hataki kwenda England.

Djuma amefunguka kwa kueleza yeye hajawahi kufika England hivyo watapambana ili kupata matokeo ili ndoto ya kufika huko ili wakipige na Everton itimie.

Kocha huyo amekiongoza kikosi hicho cha wekundu wa Msimbazi kufanya mazoezi ya mwisho leo ambapo kesho saa 9 alasiri kitacheza fainali hiyo na Gor Mahia FC.

Bingwa wa fainali hiyo atajitwalia kiasi cha fedha, shilingi milioni 60 pamoja na kugharamikiwa kuelekea England kukipiga na Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park.

No comments:

Post a Comment