Sunday, 3 June 2018

Robert Kaseko Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Atembelea Kukagua Miradi Mbalimbali ya Chama Hicho Longido

Mjumbe wa Kamati ya Siasa Halmashauri Kuu ya Ccm Mkoa wa Arusha Alipata nafasi ya kutembelea na kujionea utekelezaji wa ilani ya CCM Wilayani Longido ambayo ni wilaya ninayoiwakilisha kama Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya  Halmashauri  Kuu ya CCM  Mkoa wa Arusha.Nilitembelea  baadhi ya Miradi inayotekelezwa na Serikali Wilayani humo;     

1.Mradi Mkubwa wa Maji Longido.
Mradi Huu Utaigharimu Serikali Kiasi cha Fedha TZS Bilioni 15.8 hadi kukamilika kwake. Chanzo chake ni Mto Simba huko Wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro. 

Uzinduzi na uwekaji jiwe la msingi  ulifanywa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa mwezi Septemba, 2017. Mradi huu unasimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Arusha ( AUWSA ) na kwa hakika Maendeleo ya Utekelezaji wake ni Mazuri, inaridhisha. 

Kukamilika kwa Mradi huu Mkubwa wa Maji utaondoa Changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji kwa wanaLongido ambapo mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha Lita 2,160,000 za maji wakati mahitaji ya sasa ni Lita 1,462,000 tu. 

Nichukue nafasi hii kuipongeza sana Serikali ya Rais John Pombe Magufuli juhudi inazochukua ili kupunguza ama kuondoa Changamoto ya Upatikanaji wa Maji na kumtua mama wa kitanzania  ndoo ya maji kichwani.

 2. Mradi wa Ujenzi wa Kituo Kikubwa kipya cha Huduma za Afya  Eworendeke kata ya Namanga.
Nimetembelea  Mradi huu wa ujenzi wa  Kituo Kikubwa   cha afya  utakaogharimu Fedha za kitanzania zaidi ya  TZS Milioni 800 hadi kukamilika kwake na zaidi ya Milioni 450 zimekwisha tumika na ujenzi unaendelea. 

Nimeridhishwa na maendeleo ya Utekelezaji wake na baada ya kukamilika kwake wananchi wa Namanga na maeneo ya jirani watapata huduma  zote muhimu ikiwamo Huduma kwa wakinamama wajawazito & watoto, huduma ya X- ray, Ipasuaji n.k  

Wananchi hawatakwenda tena umbali mrefu kutafuta huduma za afya ambapo hulazimika kwenda nchi jirani ya kenya na maeneo mengine umbali mrefu ili tu kupata huduma za afya. Hongera nyingi sana kwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuboresha huduma za afya.

3. Uboreshaji wa Huduma za Afya Kituo Cha Afya Longido Mjini.
Nikiwa na Katibu wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM) Wilaya ya Longido Comrade Isaya Mollel baada ya kupokelewa na Kaimu Mganga Mkuu Dr. Jisabo Ngasa  tumetembelea Kituo Cha Afya Longido na kujionea utoaji wa huduma za afya Pamoja na kujionea Jengo jipya la huduma  ya  X- Ray na tayari ujenzi umekamilika na Mashine ya X- Ray ipo kwenye jengo hilo ikisubiri kufungwa ( Installation )  tu na mara baada ya kufungwa itaanza kutoa Huduma mara moja na  kuondoa changamoto iliyokuwepo awali ambapo huduma hii ilikihitajika ilikuwa ni mpaka mgonjwa asafirishwe Arusha mjini au nchini jirani ya Kenya. 

Pia Niwapongeze sana wadau wa Maendeleo Nchini hususani " Ngorongoro Conservation Area" kwa kujitolea kununua Jenereta mpya kubwa kwa ajili ya kuondoa/Kupunguza tatizo la Umeme pindi unapokatika.  Naipongeza sana Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli kwa kuendelea kuboresha Huduma za afya kwa watanzania na hivyo kupunguza vifo vinavyoweza epukika.

HAPA KAZI TU,  TUKUTANE KAZINI.
 
Robert PJN Kaseko
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha.
Juni 01, 2018

No comments:

Post a Comment