Monday, 4 June 2018

RC MAKONDA AGAWA KONTENA LA TENDE KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amepokea shehena ya Tende kutoka Taasisi ya Darul Irshaid Islamic kwa kushirikiana na Miraji Islamic Center Kama sehemu ya sadaka kwa waislamu katika mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhan.

==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>


 RC Makonda amesema tende hizo zitatolewa kwa vituo vya watoto yatima na waishio katika mazingira magumu vilivyopo Jijini Dar es salaam.

 Aidha RC Makonda amewasihi kinadada kuheshimu imani za watu kwa Kujisitiri na kuvaa nguo za heshima ili kuepuka kuharibia Swaumu.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Miraji Islamic center Bwana Arif Yusuph Abdulrahman amesema wameamua kutoa Tende hizo Kama sehemu ya sadaka katika mwezi wa Ramadhan.

No comments:

Post a Comment