Polisi Mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoani humo, wamekamata kiwanda bubu kinachotengeneza vinywaji vikali ambavyo vimepigwa marufuku hapa nchini.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Bwana HAMISI ISSA amethibitisha kukamatwa kwa vifaa mbalimbali vya kutengenezea pombe hizo katika nyumba  moja ya kuishi maeneo ya Msaranga Manispaa ya Moshi.

Amesema vifaa mbalimbali vya kutengeneza pombe hizo vimekamatwa zikiwemo chupa 1,600 na stika 800 zenye nembo feki za Mamlaka ya Mapato nchini pamoja na watu wawili waliokuwa wanatengeneza pombe hizo.

Naye Afisa Mwandamizi wa Kodi, Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoani Kilimanjaro, Bwana TILSONI KABUJE amesema bidha hizo hazina ubora kutokana na kutengenezwa katika mazingura ambayo siyo salama pamoja na kuziingiza sokoni bila kulipa kodi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: