Sunday, 3 June 2018

Mzee Akilimali: Kwa wachezaji wa kigeni msimu huu Okwi ndiye mchezaji bora


Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali ‘Mzee Akilimali’ amesema kwake anaona mchezaji bora wa kigeni msimu huu ni Emmanuel Okwi.

Okwi ameipa Simba ubingwa msimu uli­opita baada ya kupita miaka mitano bila kufanya hivyo huku akiibuka mfungaji bora wa ligi kuu akiwa katupia kambani mabao 20.

Mzee Akili­mali ambaye amepanga kuwania Urais wa Yanga, Okwi alikuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho na kusaidia kutwaa ubingwa huku yeye akifunga mabao mengi huku akimtaka asibadilike na kurejea tabia ya zamani ya kuomba ruhusa mara kwa mara.

“Kwa wachezaji wa kigeni msimu huu Okwi ndiye mchezaji bora, alifanya vizuri baada ya kuisaidia timu itwae ubingwa na alikuwa tishio kila alipokuwa akiingia uwanjani kuwakabili wapinzani na hata mashabiki pin­zani waliogopa kuto­kana na uwezo wake.

“Lakini ushauri wangu ni kwamba asije akayarudia yale ambayo yaliwahi kuto­kea huko nyuma siyo anapewa ruhusa siku tano yeye anakaa 20 haifai ajue yuko ka­zini na klabu yake in­amthamini ndiyo maana akawa pale. Kwa Yanga sijaona mchezaji wa kimataifa aliyefanya vyema kwa kuwa wengi walikuwa majeruhi,” alisema Akilimali.

Okwi alipotua Simba msimu uliopita alipewa Sh136 huku ikielezwa kwamba nyumba yake anayoishi Dar es Salaam anali­piwa zaidi ya Shilingi milioni 2 kwa mwezi.

No comments:

Post a comment