Mbunge wa Kibamba, John Mnyika ameiambia Serikali kuwa alipokuwa gereza la Segerea kumekuwa na matatizo ya ubambikiziwaji kesi na hali hiyo imekithiri.

Mnyika ameihoji Serikali kuwa itaanza lini kutoa fidia kwa wananchi waliobambikiziwa kesi ili utamaduni huyo ukome?amehoji.

“Nilikuwa gereza la Segerea matatizo haya ya Ubambikizwaji wa kesi yapo Tarime lakini yapo Segerea na Mahabusu nyingine, sasa kwakuwa tabia hii imekithiri magereza mengi sana ili hali hii ya kubambikiwa kesi iweze kukoma, serikali ni lini itaanza kutoa fidia kwa wananchi waliobambikiziwa kesi ili utamaduni wa kubambikiziwa kesi ukome? amehoji Mnyika leo Juni 5, 2018, Bungeni jijini Dodoma.

Akijibu kwa Niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, Antony Mavunde amesema kuwa “Amezungumza namna watu wanavyobambikiziwa kesi na kuwalipa fidia, utaratibu wa Kimahakama uko wazi wa unajieleza kabisa inapotokea mtu yoyote ameshtakiwa Mahakamani na baadae ikagundulika kwamba amebambikiziwa kesi utaratibu wa kisheria upo wa kumtaka yeye afungua kesi ya madai lakini serikali hailipi moto tu moja kwa moja. Kwahiyo wale wote wanaohisi wamebambikiziwa kesi utaratibu upo na wafuate sheria.”
Share To:

msumbanews

Post A Comment: