Baada ya kuenea kwa tetesi kuwa beki wa Yanga, Kelvin Yondani anahusishwa kujiunga na watani zao wa jadi Simba pamoja na Azam FC, Katibu Mkuu Yanga, Boniface Mkwasa, amefunguka.

Mkwasa ameibuka na kusema kuwa Yondani hana mipango hiyo huku akisisitiza kuwa bado wana mkataba naye hivyo ataendelea kusalia Yanga.

Katibu hiyo amesema taarifa zilizoripotiwa kuhusiana na Yondani kuondoka hazina ukweli wowote huku akieleza kuwa ni uzushi wa baadhi ya watu wanaotaka kuchaua picha ya klabu.

Wakati Mkwasa akiweka msisitizo kuwa Yondani bado ana mkataba na Yanga, uongozi wa klabu hiyo umeelezwa kuanza mazungumzo ili kumbakisha mchezaji huyo ndani ya timu.

Taarifa zinasema mara baada ya Yondani kukutana jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ndani ya Yanga, Hussein Nyika, imeelezwa walizungumza kufanya maboresho ya kuongeza mkataba ili beki huyo aendelee kusalia Yanga.

Beki huyo hajaungana na wachezaji wa kikosi cha Yanga kuelekea Kenya kwa ajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup yanayotarajia kuanza June 3 2018 jijini Nairobi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: