Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Bw.Charles Kabeho amemuagiza mkuu wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, Bw. Pololeti Kamando Mgema kuwakamata na kuwachukulia hatua viongozi watatu wa halmashauri ya wilaya ya Madaba akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw.Shafii Mpenda kwa tuhuma za kuhujumu na kuchakachua ujenzi wa kituo cha afya cha Madaba na kujengwa chini ya kiwango.
Ni mara baada ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Bw. Charles Kabeho kubaini tofari za simenti ambazo hazina kiwango, zilizotumika kujengea kituo cha afya cha Madaba zikiwa zimefichwa.
Wakati tuhuma hizo zikiwaangukia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba, Bw. Shafii Mpenda, Afisa Manunuzi, Bi. Betty Ng’ombo pamoja na mhandisi, Injinia Jonas Maganga, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo anasema yeye hahusiki na kuficha tofali hizo huku afisa manunuzi naye akikana kuhusika kwenye uchakachuaji wa ununuzi wa vifaa vya ujenzi.
Hata hivyo, kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Bw. Charles Kabeho akatoa maagizo kwa mkuu wa wilaya ya Songea, Bw.Pololeti Kamando Mgema
Share To:

msumbanews

Post A Comment: