Monday, 4 June 2018

Angel Mary Awatamani Vannesa na Alikiba.

Msanii wa muziki Bongo, Angel Mary amefunguka kuhusu mipango yake ya kimuziki kwa miaka ya mbeleni.

Muimbaji huyo amesema moja ya ndoto zake ni kuweza kuiwakilisha Bongo Flava na Tanzania kiujumla kimataifa kama wanavyofanya Alikiba na Vanessa Mdee.

“Angalau miaka mitatu/mitano mbeleni muziki wangu uwafikie sio Watanzania tu, sio East Afrika tu, yaani dunia nzima. Nipate kuwa mmoja wapo ya wasanii ambao tunaona kama Vanessa Mdee, Alikiba ambao wanapeperusha bendera ya Tanzania vizuri sana,” Angel ameiambia Clouds TV.

Ameendelea kwa kusema kuwa kufanya hivyo inakuwa kama chanzo cha kujivunia kuwa Mtanzania kwa kuona kwamba tunafanya kitu kizuri. Kwa sasa Angel Mary ambaye ni zao la BSS anatamba na ngoma inayokwenda kwa jina la Magongo.

No comments:

Post a Comment