Monday, 4 June 2018

Ajinyonga baada ya kunyimwa tendo la ndoa na mkewe

Mwanaume mmoja Nchini Uganda aliyetambulika kwa majina Joseph Ojur mwenye miaka 52 mkazi wa ukanda wa  Kabagu katika manispaa ya Njeru amejinyonga mpaka kufa baada ya kunyimwa ‘unyumba’ na mkewe.

Kamanda wa Polisi eneo la Njeru, Christopher Tuhunde amesema kuwa, marehemu alijinyonga ndani ya nyumba yake na jeshi hilo linaendelea kuchunguza kwa undani juu ya tukio hilo ili kuja na ripoti kamili kuhusiana na kujinyonga kwa Ojur.

“Naomba niwashauri ndugu zangu kuwa muwazi na penda kuomba ushauri kwa majirani  juu ya matatizo yanayowakabili kuliko kukimbilia kujiua”, amesema Kamanda Tuhunde

Taarifa za awali zinasema kuwa mwanaume huyo alifanya vipimo vya afya yake na kugundua kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ndipo mkewe alianza kumkatalia kufanya naye tendo la ndoa.

No comments:

Post a Comment