Friday, 11 May 2018

Yaya Toure aagwa kwa heshima Man City

Yaya Toure

HATIMAYE kiungo Yaya Toure ameagwa rasmi ndani ya Klabu ya Manchester City baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka nane.

Toure aliagwa usiku wa juzi wakati timu yake ikipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Brighton katika Premier League huku akikabidhi­wa jezi ya heshima kutoka kwa kaka yake, Kolo Toure ambaye alikaribishwa kuwa mgeni rasmi.

Akimzungumzia mchezaji huyo nahodha wa City, Vincent Kom­pany alisema: “Unapozungumzia nguli wa soka klabuni hapa, Yaya anastahili kuwa na sifa hiyo.”

Wachezaji wa City waliungana kwa pamoja kumuaga kuanzia uwanjani hadi ndani kwenye vyumba vya Uwanja wa Etihad. Katika mchezo huo, Yaya alianza katika kikosi cha kwanza akiwa nahodha na kutolewa katika daki­ka ya 86, nafasi yake ikachukuliwa na Lukas Nmecha.

No comments:

Post a Comment