Wednesday, 2 May 2018

YANGA: SIMBA HAWAJATUTOA KWENYE RELI
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa hivi sasa umewekeza nguvu zake kwenye maandalizi ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M Alger.

Yanga wameeleza kuwa matokeo waliyoyapata kwenye mechi ya ligi iliyopita dhidi ya watani zao wa jadi, Simba, hayawaharibii mipango yao wala hayawatoi kwenye reli.

Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, ameeleza kwamba mpira siku zote unakuwa una matokeo matatu hivyo yaliyotokea dhidi ya Simba wameshayapokea na yameshapita.

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuanza safari yake kesho Alhamis kuelekea Algeria kikipitia Dubai tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Alger.

Mechi hiyo ya kwanza itapigwa Mei 7 nchini humo
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Application yetu ya Msumba News ili upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.

Tumekurahisishia; 

No comments:

Post a Comment