Thursday, 10 May 2018

Yaliyojiri kwenye Baraza la Madiwani la kuwasilisha taarifa za kata za robo ya tatu 2017/18

#Kuendelea kusimamia vizuri miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya halmashauri licha ya asilimia kubwa ya miradi kuendelea vizuri .
#Wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Wakala wanaokusanya taka licha ya changamoto kubwa ya ukusanyaji taka inayotokana na uharibifu wa miundombinu ya barabara unaosababisha kuharibu hata magari ya kubebea taka hizo.
 #Kata ya Moivo wametakiwa kuanza mchakato wa kuomba kupata eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari,kutokana na kata hiyo kutokuwa na shule ya sekondari huku watoto wa eneo hilo wakisoma kwenye shule ya sekondari Olturoto shule ambayo inachukua wanafunzi wa kata tatu na kusababisha msongamano wa wanafunzi kwenye shule hiyo.
#Viongozi wa kata na vijiji , wametakiwa kuendelea kuwahamasisha wananchi kuendelea kuchangia miradi ya maendeleo katika maeneo yao huku viongozi hao wakitakiwa kusimamia vema fedha zilizochangwa na wananchi.
#Maafisa watendaji wa Kata wametakiwa kuwasimamia Watendaji wa vijiji, kuhakikisha Mikutano Mikuu ya vijiji inafanyika na wananchi wanasomewa taarifa za mapato na matumizi.
#Wakala wa Barabara mijini na vijiji 'TARURA' wanapita kwenye kata na kubainisha hali halisi ya miundombinu ya barabara zote kwa lengo la kuweka mkakati wa  kuzitengeneza.    
#Maafisa watendaji wa kata, kuacha kujishirikisha kwenye masuala ya siasa ambazo kimsingi zinaleta changamoto katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya wananchi katika maeneo yao.
Katika mkutano huo Madiwa wa kata waliwasilisha taarifa za utekelezaji ya shughuli za maendeleo kwa kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2017/18, huku kata nyingi zikikabiliwa na changamoto ya uharibifu wa miundombinu ya barabara unaotokana na mvua zinazoendelea kunyesha sambamba  na wadudu waharibifu wa nashambuli mimea ya mazao ya chakula shambani. 

No comments:

Post a comment