Thursday, 3 May 2018

Waziri Mkuu atoa onyo kali kwa TRA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameionya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuacha kutumia lugha zenye kuudhi wananchi pindi wanapokwenda kukusanya kodi kwa wafanyabiashara katika maeneo yao ya kazi pamoja na kutowatoza kodi kubwa ambayo haina uhalisia.

Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Mei 03, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 21 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la Mbunge rank Mwakajoka aliyetaka kujua Serikali inatoa kauli gani kuhusu matatizo wanayofanyiwa wafanyabishara na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

"Wafanyabiashara wote kwanza wawe na amani katika kufanyabiashara zao nchini na wawekezaji wote waendelee kuwekeza na kuongeza mtaji zaidi ili kuekeza zaidi kwa sababu serikali imedhamiria kufungua milango ya uwekezaji nchini. Tunajua kwamba kodi ni wajibu wa kila mmoja kadiri ya shughuli zake zinazomletea mapato ilivyo kwa ukubwa wake. Kwa hiyo tumeielekeza TRA ihakikishe inapokwenda kukusanya kodi haitumii lugha ya kuudhi wala nguvu", amesema Majaliwa.

Pamoja na hayo, Majaliwa ameendelea kwa kusema "ndio maana tulianzisha kitengo cha elimu ndani ya TRA ikiwa na lengo la kumuelimisha mwananchi umuhimu wa kulipa kodi, hakuna sababu ya kumlazimisha mlipa kodi. Pale patapotokea malalamiko wafanyabiashara wana uhuru mkubwa wakuenda kwa kiongozi mkubwa wa eneo hilo ili kulalamikia jambo hilo ili sheria zipate kuchukuliwa".

Kwa upande mwingine, Waziri Majaliwa amesema serikali haina ugomvi na wafanyabishara na TRA wanapaswa kufanya kazi vyema huku akiwaomba wafanyabiashara kutoa taarifa pindi wanapobughudhiwa na TRA wasiwapandishie, kodi wafanyabiashara

No comments:

Post a Comment