Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Maxwell Stanslaus  akizungumza na Mkazi wa Arusha katika zoezi la uchangiaji wa damu lililoendeshwa ma taasisi yake.
Wanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Rodgers Nelson   wakichangia damu katika viwanja vya Sheikjh Amri Abeid
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
 Taasisi isiyokua ya kiserikali ya Wanaume inayojulikana kama Men At Work imeendesha zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya kinamama wanaojifungua na kupoteza damu nyingi pamoja  majuruhi wanaonusurika na ajali na kufikishwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru .

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Maxwell  Stanslaus amesema kuwa wameamua kuwa wameamua kuchangia damu  kama mchango wanaume kujitoa kwa ajili ya jamii na kuisaidia jami kwasababu wanaume ni nguzo ya familia,jamii na taifa kwa ujumla.

Max aliwataka wanaume wote nchini kuwajibika na kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii .

“Kwa sasa  tumeamua kushirikiana na kitengo cha damu salama kuchangia damu ili kupunguza changamoto ya upungufu wa damu katika benki ya damu “ Alisema Max

Max alisema kuwa taasisi hiyo ina kazi kuwa ya kuwahasisha wanaume kuwa wawajibikaji na kushiriki katika nafasi za malezi  familia na jamii ili kujenga familia imara na hatimaye taifa imara.

Kwa upande wake Mwanachama wa Men At Work Rodgers Nelson alisema kuwa anajisikia faraja kuchangia damu  ili kusaidia kuokoa maisha ya kinamama wajawazito ambao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.

Naye Shemeji Melayeki  alieleza kuwa ni mara yake ya kwanza kutoa damu hivyo amewatoa hofu wananchi kutokua waoga wa kuchangia damu kwani zoezi hilo linafanyika kwa umakini na halina madhara yoyote.
 Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Application yetu ya Msumba News ili upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.

Tumekurahisishia; 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: