Tuesday, 22 May 2018

Ripoti ya tume ya kuchunguza mali za CCM nchi nzima yatua mikononi mwa Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Mei 21, 2018 amepokea ripoti ya tume maalumu ya kufanya uchunguzi wa mali za Chama cha Mapinduzi (CCM) nchi nzima, katika Ofisi ndogo za Chama hicho zilizopo Lumumba jijini Dar es salaam.
Rais Dkt. John Magufuli
Tume hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ilipangwa mwaka jana mwezi Desemba jijini Dodoma na Rais Magufuli mapema baada ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, ili kufuatilia mali zote za chama hicho nchi nzima.

No comments:

Post a comment