Tuesday, 1 May 2018

Rais waTFF Wallace Karia atoa onyo kwa klabu zote zitakazo wasajili vijana wa Serengeti Boys


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia amezitaka klabu zote zitakazo wachukua wachezaji wa Serengeti Boys kuhakikisha wanapata nafasi ya kucheza kwenye timu zao huku akitarajia kuweka sheria kali kwa wale watakao shindwa kuwachezesha.

Karia ameyasema hayo wakati wa mapokezi wa mabingwa hao wapya wa michuano ya kombe la CECAFA  baada ya kuichapa timu ya taiafa ya Somalia kwa jumla ya mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali Aprili 29, 2018 mjini Bujumbura nchini Burundi.

No comments:

Post a Comment