Monday, 21 May 2018

Picha 7 : Wasaidizi wa Makamu wa Rais, wawakumbuka yatima Dodoma

Wasaidizi wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametoa futari kwa kituo cha watoto Yatima cha Rahman kilichopo Chang’ombe Dodoma.
Kituo hicho chenye watoto 120 ambao kati ya hao 75 ni yatima ambapo hupatiwa Elimu ya Dini na Lugha.
Wasaidizi hao ambao waliwakilishwa na Kaimu Katibu wa Makamu wa Rais Bi. Maulidah Hassan na Msaidizi wa Masula ya Siasa Ndugu Nehemia Mandia kwa pamoja walisema imekuwa utamaduni wao kukutana, kuzungumza na kusaidia watoto yatima, watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na walemavu na wameahidi kuendelea kusaidia kila inapowezekana.
Kwa upande wake, Mwanzilishi wa Kituo hicho Bi. Rukia Hamisi ameshukuru kwa wasaidizi wa Mheshimiwa Makamu wa Rais kufika ofisini kwake na ameomba Mheshimiwa Makamu wa Rais akipata nafasi naye afike kituoni kwani watoto wanampenda sana pili alishukuru kwa futari.
Tazama picha zaidi:
No comments:

Post a comment