Thursday, 31 May 2018

Ndoa ya Majey na Lulu mbioni


Stori zilizopo kwa sasa huwenda ndoa ya Majey na Lulu ipo mbioni kufungwa.

Mtu wa kwanza kuweka wazi hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

Nikiwa mwenyekiti wa kamati ya harusi ya ndugu Majizo na Bibi Elizabeth Michael(Lulu) nimeupitisha huu wimbo wa Mrisho Mpoto na Harmonize kua ndo wimbo rasmi wa harusi yao, tarehe za harusi endelea kufuatilia 92.5 Dodoma @majizzo @elizabethmichaelofficial

Wimbo aliopitishwa na RC Makonda ni wa Mrisho Mpoto ‘Nimwage Radhi’ ambao amemshirikisha Harmonize.

April 2017 katika mahojiano na gazeti la Mtanzania, Lulu alisema siku za ndoa yake na Majey zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa itatangazwa kwa uwezo wa Mungu na hapo ndipo waliotamani waachane wataziba midomo, maana anatarajiwa kuwa mke halali hivi siku za usoni.

No comments:

Post a comment