Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amesema kumiliki biashara au kuwa na leseni ya biashara si kigezo cha kuamua kama mwanafunzi anastahili kupata mkopo au asipate mkopo

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mijini Dodoma kufuatia taarifa ambazo zimesambaa kwenye vyombo mbalimbali pamoja na mitandao ya kijamii zikieleza kuwa wafanyabiashara wenye leseni watoto wao hawatapata mikopo kwa ajili ya Elimu ya Juu.

Amesisitizama kinachoangaliwa ni kipato ambacho mzazi au mlezi anakipata katika kazi anayoifanya kama kinaweza kumgharamia mtoto wake masomo ya Elimu ya Juu na sio kazi anayoifanya.

Naibu Waziri Ole Nasha amewataka wananchi kupuuza taarifa hizo za uongo na upotoshaji zenye lengo la kuvuruga utaratibu uliopo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikali
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
11/05/2018





Share To:

msumbanews

Post A Comment: