Tuesday, 15 May 2018

Mwakyembe awapa changamoto Wajumbe wa bodiWaziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, amewapa changamoto wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Michezo Malya, ambao amewateua hivi karibuni ya kuhakikisha wanawasaidia vijana wenye ari ya michezo.

Mwakayembe ametoa changamoto hiyo kwenye uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika mapema leo Mei 15, kwenye chuo hicho huko Malya, Kwimba, Mwanza. Amesisitiza kuwa wanatakiwa kujitoa kwaajli ya kuhakikisha taifa linapiga hatua katika michezo.

"Nataka niwaambie wajumbe wa Bodi hii changamoto ya kwanza inayowakabili ni kuhakikisha taasisi hii yenye wajibu adhimu katika maendeleo ya michezo mnaitangaza na kuiongezea thamani ili iweze kuhudumia Vijana wenye ari ya kupata ujuzi katika michezo", amesema.

Aidha Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa ndoto yake ni kukiona chuo cha Malya kinakabiliwa na mafuriko ya wanachuo kuliko uwezo wake ili waweze kuingia makubaliano yenye tija na taasisi za kifedha na wadau wa michezo kuwekeza kwenye viwanja vya michezo na walimu zaidi.

Chuo cha Malya ndio chuo pekee nchini kilicho chini ya serikali amabcho kinatoa elimu ya michezo kwenye maeneo tofauti ikiwemo Uongozi kwenye taasisi za michezo pamoja mafunzo ya waamuzi.

No comments:

Post a comment