Arsenal wameimarisha ofa yao kwa kiungo wa kati Jack Wilshere. Mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 26 unafikia kikomo mwisho wa msimu na amekuwa akitafutwa na Wolves na Everton. (Mirror)
Mchezaji anayesakwa sana na Liverpool Max Meyer hatachezea tena Schalke baada yake kufukuzwa kutoka mazoezini na kutoka kwenye kikosi cha kwanza. Meyer, mshambuliaji mwenye miaka 22, aliadhibiwa baada yake kumkosoa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Bundesliga Christian Heidel. (Sky Sports)
Rais wa Real Madrid Florentino Perez amesema Gareth Bale, 28, anataka kusalia Bernabeu licha ya tetesi kwamba huenda mshambuliaji huyo wa Wales akahama. (Sun)
Pep Guardiola amesema uamuzi ufaao utafanywa kuhusu kipa wa Manchester City Joe Hart iwapo West Ham wataamua kutobadilisha mkataba wake wa sasa wa mkopo kuwa uhamisho wa kudumu. (Mirror)
Marouane Fellaini, 30, anataka Manchester United wampe mkataba wa muda mrefu zaidi kushinda mwaka mmoja ambao wamemuahidi kwa sasa Old Trafford. (ESPN)
Kiungo wa kati wa Arsenal Santi Cazorla anatumai kwamba ataweza kurejea kucheza kabla ya mwisho wa msimu. Mhispania huyo mwenye miaka 33 hajachezea Gunners tangu mwaka 2016 kutokana na jeraha la mguuni ambalo limekosa kupona. (AS)
Meneja wa Shakhtar Donetsk Paulo Fonseca amekataa ofas kutoka kwa Everton baada ya kuanza kuangazia kumrithi Arsene Wenger Arsenal, kwa mujibu wa mwanahabari Guillem Balague. (Express)
Thierry Henry na Tony Adams ni miongoni mwa watu mashuhuri 100 wa Arsenal ambao wamealikwa kwa mechi ya mwisho ya Wenger nyumbani, ambapo watasherehekea miaka 22 ya Mfaransa huyo katika klabu hiyo. (Mail)
Mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll, 29, alifukuzwa kutoka mazoezini Jumatatu na meneja wa klabu hiyo David Moyes baada ya wawili hao kukorofishana. Klabu hiyo inatarajiwa kuanza uchunguzi kuhusu kisa hicho. (Telegraph)
Imeandaliwa na BBC
Share To:

msumbanews

Post A Comment: