Saturday, 26 May 2018

MBARAZA UVCCM DAR ATEMBELEA SIDO.Mjumbe wa Baraza la Kuu Taifa UVCCM kupitia Mkoa wa Dar es salaam Ndg Gwantwa Alex Mwakijungu akisindikizwa na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Temeke Ndg Fadhili Muhamed wametembelea ofisi za SIDO (Small Scale Industrial Development Organization), _Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo_ Mkoa wa Dar es salaam na kufanya mazungumzo na Meneja wa SIDO Mkoa wa Dar es salaam Bw. Mack Donald Maganga juu na namna mbalimbali ambazo Shirika hilo litaweza kusaidia vijana Mkoa wa Dar es salaam katika kuwainua kiujuzi na maarifa ili kufikia malengo ya Dar es salaam ya Viwanda.

==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>


Katika mazungumzo hayo Bw Maganga amekubaliana kushirikiana kwa pamoja na Mjumbe wa Baraza UVCCM Dar es salaam Ndg Gwantwa Alex katika kuandaa programu maalum ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wa CCM ambao watapokelewa na kupewa mafunzo ya fani mbalimbali kama njia ya kuunga mkono sera ya Tanzania ya Viwanda na kuwawezesha kiuchumi.

Programu hiyo maalum ya mafunzo itaanza rasmi mapema mwezi wa sita mwaka huu baada ya taratibu za kiutendaji za pande zote mbili za makubaliano zitakapo kamilika.

'' UVCCM DAR ES SALAAM, TUKUTANE KAZINI"

No comments:

Post a comment