Saturday, 5 May 2018

Manara amwagia sifa Ajib

Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa vinara wa Ligi Kuu (VPL) Simba SC, Haji Manara amefunguka na kumwagia sifa nyota wa Yanga Ibrahim Ajib kuwa ni mchezaji bora na mwenye kipaji kilichokuwa kizuri zaidi nchini huku akiwataka mashabiki wa Yanga kuacha kumtolea maneno ya fedheha mchezaji huyo.

Manara ametoa kauli hiyo leo asubuhi Mei 05, 2018 kupitia ukurasa wake maalum wa kijamii baada ya kuwepo taharuki kubwa kwa mashabiki wa soka hasa ya wa Yanga kuvurugwa akili zao juu ya kitendo cha mchezaji huyo pamoja na wenzake watatu kutoweza kuungana na kikosi kilichosafiri juzi kuelekea nchini Algeria licha ya uongozi wa Yanga kutoa sababu zenye umuhimu wa kutoshiriki wachezaji hao.

"Ni kukosa heshima kuliko pitiliza, ni kukosa shukrani na heshima kuna kofaa kukemewa na wadau wote. Kwangu mimi Ajibu ni kipaji maridhawa zaidi nchini kilicho hai hakuna gundu wala nundu", amesema Manara.

Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "yeye alipe mishahara ya wachezaji? atengeneze morali kwenye timu? kafunga magoli mangapi msimu huu? 'assist' alizofanya hamkuziona ?. Pole dogo ila hao ndio 'gongowazi' bro".

Kwa upande mwingine, Manara amempa ushauri mzito Ibrahim Ajib kuwa endapo ataona mambo yamezidi kuwa magumu huko alipo sasa basi asisite kurudi Simba SC kwa kuwa alivyoondoka hakuua mtu yeyote aliondoka kwa amani na upendo juu yake.

No comments:

Post a Comment