Friday, 11 May 2018

Manara amwaga cheche baada ya Simba kuwa mabingwa rasmi wa ligi kuu ‘haki imechelewa’

Afisa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara ameanza kuongea baada ya Yanga kuvuliwa taji rasmi la ligi kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2017/18.
Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa instagram, Manara ameandika kuwa haki imechelewa huku akimshukuru Mungu kwa kufanikiwa kutwaa taji hilo.
Sifa ziende kwa Mwenyezimungu Mwingi wa Rehma..muumba mbingu na ardhi..niseme nn zaidi ya hapo?
We are…..
We are
Haki imechelewa ila Mungu huyu ni wetu sote…..🙏🏅🏆
Wekundu wa msimbazi Simba wametwaa ubingwa huu mara ya mwisho ikiwa ni msimu wa mwaka 2011/12 kisha Yanga msimu wa mwaka 2012/13 na Azam FC mwaka 2013/14 kisha Yanga ikatwaa tena mfululizo msimu wa mwaka 2014/15, 2015/16 na 2016/17 na sasa vijana wa Simba wanasema Simba yao, mwaka wao.

No comments:

Post a Comment