Naibu  Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akizungumza na wananchi wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji (hawapo pichani), kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde akifafanua jambo kwa wananchi wa Kata ya Miyuji, Makutupora, Msalato na Nzuguni waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.



 Wananchi wa Kata ya Miyuji, Makutupora, Msalato na Nzuguni wakimsikiliza kwa makini Naibu  Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa (hayupo pichani), kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.


 Naibu  Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akisalimiana na wazee wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji mara baada ya kuzungumza nao kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.


 Naibu  Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi wake wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji mara baada ya kuzungumza nao kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.


 Naibu  Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akisalimiana na mmoja wa wananchi wake wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji mara baada ya kuzungumza nao kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.
 Naibu  Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akimsikiliza mmoja wa wazee wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji alipokuwa akiwasilisha malalamiko yake kuhusu kuchelewa kulipwa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.
 Mmoja wa wananchi wa Mtaa wa Mpamaa Kata ya Miyuji akizungumza mbele ya viongozi kuhusu ucheleweshwaji wa fidia ya wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.

...............................................................................................................
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa akiwa na Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde leo wamekutana wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Msalato Dodoma na kuwatoa hofu kuwa serikali itawalipa fidia zao.
Wananchi hao ni kutoka Mpamaa, Msalato, Makutupora, Miyuji na Nzughuni.

Akizungumza na wananchi hao, Kwandikwa amesema serikali inatambua madai yao na kwamba fidia zao zitalipwa kwa kuzingatia sheria za utwaaji ardhi. Amefafanua anaelewa wapo wananchi 1,470 ambao mwaka 2007/8 wamelipwa kiasi cha sh.bilioni 1.6.

Aidha amesema mwaka 2013 wananchi 980 walitathiminiwa ambapo kiasi cha sh.Bilioni 3 kilihitajika kwa ajili ya kuwalipa fidia. “Ndugu zanguni ni takribani miaka 5 sasa imepita, muda huo ni mrefu niwatoe hofu tu sheria zipo tutazizingatia,"amesisitiza

Kwandikwa amesema katika kuhakikisha wanalifanyia kazi hilo kwa haraka watashirikiana na wadau wote wanaohusika ili taratibu za ulipaji wa fidia zianze kwa mapema. Kwandikwa amesema wataangalia kama kuna sehemu watu wamechelewesha mchakato huo kwa uzembe hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao.

Awali, akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, amesema wananchi hao tangu mwaka 2009 maeneo yao yalichukuliwa lakini hadi sasa hawajalipwa fidia.

 "Suala hili wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu niliahidi kulifuatilia hili,nilikueleza suala hili nashukuru umekuwa msumbufu kwangu wa kutaka kujua lini unakuja kuzungumza na wananchi hawa, nikushukuru sana wewe na meneja wa Tanroads mkoa, kwa kuwa sehemu ya msaada kwangu,"amesema mbunge huyo.

 Mavunde amempongeza Rais John Magufuli kwa kulijenga jiji la Dodoma kwa miundombinu mbalimbali na kusema hatua hiyo inaipa hadhi zaidi jiji hilo.

 Kwa upande wao, wananchi wameiomba serikali kuiangalia upya fidia watakayoilipa ili iendane na hali ya maisha ilivyo sasa kwa kuwa ni muda mrefu tangu wafanyiwe tathimini.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: