Mwakilishi wa Jimbo la Jang’ombe visiwani Zanzibar, Abdallah Maulid Diwani amevuliwa uanachama wa CCM na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), kwa kosa la kukiuka maadili ya chama cha Mapinduzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole, Mwakilishi huo wa Jimbo la Jang’ombe, amefukuzwa uanachama kwa kwenda kinyume na maadili na miiko ya viongozi wa CCM.

“Kikao pia kimetoa karipio kwa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki, Fancy Nkuhi na Mariam Ussi Yahya kwa mwenendo usioridhisha, usiolinda maslahi ya nchi na unaokinzana na misingi na miiko ya uongozi na wamewekwa chini ya uangalizi wa kimaadili kwa miezi 18,” imesema taarifa hiyo ya Polepole.

Katika kikao hicho Rais John Magufuli pia imeazimia mapendekezo yote ya Tume ya Rais ya uhakiki wa mali za chama yafanyiwe kazi mara moja na chama chenyewe chini ya Baraza la Wadhamini na Uongozi wa Katibu Mkuu, wenyeviti na makatibu wakuu wa jumuia zake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: