Tuesday, 15 May 2018

KIKOSI CHA SIMBA CHAPEWA MAPUMZIKO MAFUPI, KESHO KUANZA KAZI MAALUM YA KAGERA

Baada ya kuwasili usiku wa jana kikitokea jijini Dodoma, kikosi cha Simba kimepewa mapumziko mafupi leo kabla ya kuendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar.

Kikosi hicho jana kilipata wasaa wa kuwasili katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia mwaliko maalum wa Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai.

Simba walipata mwaliko huo baada ya kutwaa ubingwa ligi ambao waliokuwa hawajaupata kwa muda mrefu ikiwa ni takribani miaka mitano.

Baada ya kuwasili Dar, wachezaji wa timu hiyo leo wamepata mapumziko mafupi leo Jumanne ambapo kesho kitaanza mazoezi rasmi kwa kazi maalum ya Kagera mwishoni mwa wiki hii.

No comments:

Post a comment