Sunday, 27 May 2018

KICHUYA OUT SIMBA KAHEZA IN


Msimbazi, Shiza Kichuya.

STRAIKA wa Majimaji, Marcel Boniventure Kaheza, tayari amemalizana na Simba lakini staa wa Msimbazi, Shiza Kichuya amesema mambo yake yakikaa sawa anang’oka muda wowote kwenda nje kucheza.

Kichuya anasema amesikia maoni ya baba yake mzazi akimtaka kuondoka kwenda nje kucheza soka la kulipwa na lenye masilahi zaidi na amesema analifanyia kazi kwa nguvu zote. Ngoja tukupe kwanza ishu ya Kaheza ilivyokuwa.

Simba leo Jumamosi inasafiri kwenda Songea kucheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Majimaji huku Kaheza ambaye amefunga mabao 13 kwenye ligi naye akiondoka leo kurejea kwenye kazi yake.

Kaheza, juzi Alhamisi alitua jijini Dar es Salaam kwa ndege akitokea Songea tayari kwa ajili ya kuzungum­za na mabosi wa Simba na taarifa zinasema kila kitu kimekwenda vizuri.

Chanzo chetu ndani ya Simba kilisema; “Baada ya kutua uwanja wa ndege, alifuatwa na kiongozi mmoja wa Simba kwenda kuzungumza naye na walikubaliana kila kitu, kinacho­subiriwa ni dirisha tu kufunguliwa, kila kitu kitawekwa wazi kwani mkataba wake na Majimaji unamal­izika mara tu ligi itakapomalizika.”

Championi Jumamosi lilipomtafu­ta straika huyo alisema; “Nipo Dar na nimekuja jana (juzi) Alhamisi kwa ndege kwa ajili ya kuzungumza na Simba. Kwa sasa ni mapema kusema tulichoongea, lakini dirisha la usajili litakapofunguliwa tu, itafahamika.” Usajili wa dirisha dogo un­aanza Juni 15.
Kichuya sasa Out Simba
Kichuya amesema yupo tayari kuondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu huu iwapo mambo yake yatakwenda vizuri.

Kichuya alijiunga na Simba msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mti­bwa Sugar huku akiripotiwa kupokea mshahara wa Sh Mil 1.8 katika kikosi cha Simba licha ya kuwa ni mchezaji muhimu kikosini humo.

“Suala la mkataba mpya na Simba siwezi kuliongelea kwa sababu bado sijamaliza mkataba wa kwanza hadi hapo utakapokwisha nitaweka wazi, kweli baba yangu amesema nikacheze nje ni sawa kwa sababu ni maoni yake kama mzazi maana anaona akina Simon Msuva, Mbwana Samatta na Abdi Banda wakifanya vizuri nje.

“Najua hilo limekuwa likimuumiza lakini hata mimi napambana kufanya vizuri ili niweze kupata nafasi ya kwenda kucheza nje na hilo ndiyo lengo kubwa la kujituma kwa sababu nataka kuondoka hapa nilipo na wakati wowote kutoka sasa iwapo mipango yangu itafanikiwa kwenda vizuri,” alisema Kichuya.

No comments:

Post a Comment