Wednesday, 2 May 2018

KENYA YAONGEZA MISHAHARA KWA WATUMISHI

SERIKALI ya Kenya imetangaza ongezeko la asilimia 5 kwa kima cha chini cha mshahara ili kuwalinda wafanyakazi na mfumuko wa bei ambao umefikia asilimia 4.8 mwaka huu.

Ongezeko hilo la mshahara limetangazwa na Waziri wa Ajira na Mafao ya Kijamii, Ukur Yattani wakati akisoma hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta katika Viwanja vya Uhuru Park wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) leo, Mei 1, 2018.

Aidha, Serikali ya Kenya imebaini upotevu wa masaa ya uzalishaji yaliyofikia milioni 100 kutokana na migomo ambayo ni mbaya kwa taifa hilo linaloendelea na kuona umuhimu wa kufanya mdahalo wa kitaifa na wadau ili kumaliza tatizo hilo sugu nchini humo.
 Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Application yetu ya Msumba News ili upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.

Tumekurahisishia; 

No comments:

Post a Comment