Sunday, 20 May 2018

Kauli ya Manara baada ya kufungwa na Kagera Sugar


Baada ya Kagera Sugar kutibua sherehe za ubingwa Simba jana kwa kuifunga bao 1-0 mbele ya Rais Magufuli, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara, amesema kipigo hicho wala si ishu kwao.

Manara alieleza hayo kwa kusema kuwa lengo kubwa ilikuwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara lakini suala la kufungwa jana wala halileti hasara yoyote kwasababu tayari wameshachukua ubingwa msimu huu.

"Kufungwa na Kagera wala si ishu, sisi tulihitaji ubingwa wa ligi pekee, hayo mengine yaliyojitokeza wala hayaleti kutuletea shida, bingwa ni Simba'' alisema Manara.

Simba iliiadhimia kutengeneza rekodi nyingine ya kumaliza ligi bila kufungwa lakini ilishindwa kutimia baada ya Kagera kuitibua jana.

Mchezo mwingine utakaofuatia na wa mwisho kwa Simba katika msimu huu wa ligi, utakuwa ni dhidi ya Majimaji FC utakaochezwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

No comments:

Post a comment