Tuesday, 29 May 2018

Juma Nature aachia ngoma mbili kwa mpigo, aponda uamuzi wa Q Chief kuacha muziki

Msanii mkongwe wa muziki, Juma Nature baada ya ukimya wa miaka 3 ameachia nyimbo mbili kwa mpigo kwaajili ya kuwaburudisha mashabiki wake ambao walimmiss kwa miaka mingi.
‘Nadhani’ ni mmoja kati ya nyimbo hizo zilizoachiwa Jumanne na kusikilizwa kwa mara ya kwanza kupitia kipindi cha XXL cha Clouds Fm.
Akizungumza na kituo hicho cha redio, Nature alizungumzia ukimya wake namna alivyoipokea kauli ya Q Chief kuacha muziki.
“Mimi nilimsikiliza Q Chief mwanzo mwisho, alikuwa anazingua,” alisema Nature “Mtu ambaye anafanya muziki kwa miaka yake yote hawezi kuacha muziki kwa namna hiyo labda unaweza kukaa kimya kutokana na mambo fulani halafu baadae unarejea,”
Katika hatua nyingine mkongwe huyo alidai yupo tayari kujiunga na kundi lolote la muziki likiwemo kundi la TKM ambalo alifanya nalo kazi kipindi cha nyuma.
Pia alisema wasanii ambao angependa kuunda nao kundi ni Stamina kutoka Rostam pamoja na G.Nako kutoka kundi la Weusi

No comments:

Post a comment