Saturday, 19 May 2018

Jerry Muro Aomba jezi ya Ubingwa Simba

Wakati Simba ikiwa inajiandaa kuupokea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu mbele ya Rais Magufuli, Afisa Habari wa zamani wa Yanga, Jerry Muro, ameomba jezi ya ubingwa Simba.

Mapema jana wakati wa kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Waandishi wa Habari, Makonda alimueleza Msemaji wa Simba, Haji Manara kuwa Muro anahitaji jezi hivyo ni vema akafanya utaratibu wa kumpatia.

Muro amemua kufanya uzalendo wa kuwapongeza Simba kutokana na msimu huu kuwa bora kwa kila kitu huku wakifanikiwa kuchukua ubingwa bila kupoteza mchezo wowote katika ligi.

Hii si mara ya kwanza kwa Muro kuvaa jezi ya Simba, ikumbukwe hata siku kadhaa zilizopita Msemaji huyo wa zamani wa Yanga alivaa jezi hiyo na kuweka katika kurasa za mitandao yake ya kijamii akiwapongeza watani zake mapema tu baada ya kutangazwa kuwa mabingwa wa msimu huu.

Simba itakuwa inacheza na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mechi itakayoenda na hafla ya kukabidhiwa kombe na Rais Magufuli kuanzia majira ya saa 8 mchana.

No comments:

Post a comment