Thursday, 24 May 2018

HATIMAYE INIESTA ASAINI KOBE YA JAPAN

STAA wa Soka duniani kutoka Barcelona ya Hispania, Andrés Iniesta amesaini kandarasi ya kujiunga na Klabu ya Soka ya Vissel Kobe ya nchini Japan na kukabidhiwa jezi namba 8​.
Kiuongo huyo mwenye umri wa miaka 34, bado yupo kwenye kikosi cha Hispania kilichotangazwa na Kocha Julen Lopetegui kuwania Kombe la Dunia mwezi ujao.
Andrés Iniesta amejiunga na klabu hiyo iliyopo Ligi Kuu ya Japan ‘J1 League ‘baada ya kuachana na klabu yake ya FC Barcelona aliyoitumikia kuanzia enzi za utoto wake na kutwaa mataji 34.

No comments:

Post a comment