Monday, 14 May 2018

Hamisa Mobetto ajibu kuhusu kufunga ndoa na Diamond


Mwanamitindo Hamisa Mobetto amejibu iwapo yupo tayari kufunga ndoa Diamond Platnumz mara baada ya muimbaji huyo kuweka wazi atafanya hivyo mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi wa Filamu ya Mama kutoka kwa Aunt Ezekiel, Hamisa alipoulizwa iwapo yupo tayari kuolewa na Diamond alijibu kwa sasa huwezi kuzungumzia hilo.

“Siwezi kujibu hilo swali,” aliongea Hamisa kwa kifupi.

Katika hatua nyingine Hamisa alidai kuwa yeye sio single mother kwani wazazi wenzie wanamsaidia katika malezi ya watoto.

“You can’t call your self Single Mother kama unasaidiwa kulea mtoto na baba watoto wako, so facts is mababa watoto wangu wote wananisaidia kulea watoto vizuri, kwa hiyo siwezi nikasema single mother sababu nasaidiwa kulea watoto,” amesema Hamissa.

Hamisa ni mama wa watoto wawili ambao wa kwanza alizaa na Majay na wapili alizaa na Diamod Platnumz.

No comments:

Post a comment