Thursday, 31 May 2018

Dkt. Kijo-Bisimba atangaza kazi yake mpya

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ambaye amebakiza siku chache kung'atuka kwenye nafasi hiyo Dkt. Helen Kijo-Bisimba amedai akitoka hapo ataenda kujihusisha na masuala ya uimbaji kwaya kwenye kanisa ambalo huwa anafanya ibada.

Dkt. Kijo-Bisimba ametoa wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha East Africa Drive kilichorushwa Mei 30, 2018 kutoka East Africa Radio zikiwa zimepita takribani siku tatu tokea kituo hicho kutangaza hadharani kustaafu kwa Mkurugenzi huyo pamoja na mtu ambaye atashika nafasi yake mara atakapoondoka rasmi mwanzo mwa mwezi Julai.

"Kusema ukweli mpaka sasa hivi natamani tu kupumzika. Mimi ni muimbaji wa kwaya hivyo nataka nitumie muda mwingi katika kufanya kazi zangu za kanisani, najua kabisa bado nitaendelea kushauri kazi yangu niliyokuwa nafanya", amesema Dkt. Kijo.

No comments:

Post a Comment