Mkuu  wa  wilaya ya  Same  mkoani Kilimanjaro  Rosemary  Senyamule akikagua mradi wa maji katika  wilaya ya Same 














Mkuu  wa  wilaya ya  Same  Rosemary  Senyamule  akitoa maagizo ya  kutaka mradi wa maji Hedaru kukamilika haraka
......................................................................................................................................................
MKUU  wa  wilaya ya Same  mkoani Kilimanjaro  Rosemary Senyamule amemtaka  mkandarasi  wa mradi  wa maji Kijiji  cha Hedaru  kukamilisha mradi huo unaogharimu  bilioni 1.18 ifikapo Mei 30  mwaka  huu.

Akitoa agizo hilo  wakati wa  ziara  yake ya  kukagua  mradi huo juzi mkuu  huyo wa  wilaya  alisema lengo la  serikali ya  awamu ya  tano inayoongozwa na Rais Dkt  John Magufuli ni kuona mwanamke anatua  ndoo  kichwani  kwa kupata  huduma  ya maji .

 Alisema  mradi  huo  umelenga  kufikia  vijiji 10 ambao ulitakiwa kukamilika  toka  mwaka  2015 ila  hadi  sasa  umekuwa  ukienda  kwa  kusuasua .

Hivyo  alimtaka  mkandarasi kuhakikisha maji yanatoka sasa  wakati wa kiangazi kwani wananchi wamekuwa wakihofu kama kweli mradi utatoa maji wakati wa kiangazi.

" Naitaka kamati iliyoundwa kusimamia maji  kukagua maeneo yote na kutoa taarifa kwa mhandisi  kabla mkandarasi hajakabidhi ili akabidhi mradi usio na kasoro"

Hata  hivyo  alisema katika  ukaguzi  alioufanya katika mradi huo  amebaini mifumiko mingi imevunjika, koki nyingi zimeibiwa.


"Mji wa Hedaru ni mji unaaongoza kwa kukua kwa kasi Wilayani Same Mhandisi Mussa aeleza jinsi mradi huo utakavyoongezewa nguvu na tanki lingine linalojengwa mwaka huu, ili kukidhi ongezeko la watu"

Alisema  kuwa mradi huu ni kati ya miradi iliyokuwa imeainishwa kwenye ilani ya CCM 2010- 2015 hivyo atakayecheza nao atawajibishwa vikali .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: