Thursday, 31 May 2018

Bashiru akabidhiwa Ofisi na Kinana


 Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo Alhamisi Mei 31, 2018 amemkabidhi ofisi mrithi wake Dk Bashiru Ally, katika ofisi ndogo za chama hicho tawala, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Baada ya makabidhiano hayo, wawili hao wameingia katika kikao cha ndani na wafanyakazi wa chama hicho.

Dk Bashiru anakuwa Katibu Mkuu wa nane wa CCM baada ya kujiuzulu kwa Kinana aliyemuandikia barua mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli aridhie ombi lake hilo.

Mei 29, 2018 Halmashauri Kuu, ambayo ni chombo cha pili kwa ukubwa cha CCM na ambayo ilikutana kwa siku mbili Ikulu jijini Dar es Salaam, ilimpitisha Dk Bashiru ambaye aliongoza kamati iliyohakiki mali za chama hicho kwa miezi mitano kuwa katibu mkuu mpya wa chama hicho.

No comments:

Post a comment