Thursday, 31 May 2018

AZAM FC YAMTANGAZA PLUIJM RASMI, YAWEKA AHADI YA KUTANGAZA KIFAA KIPYA JUMATATUUongozi wa Azam FC, leo umemtangaza rasmi kocha Hans van der Pluijm.

Pluijm amejiunga na Azam FC akitokea Singida United na blog hii ilieleza kuhusiana na kujiunga na Azam FC.

Azam FC ilikuwa kimya kuhusiana na suala hilo hadi leo ilipotangaza kupitia Msemaji wake, Jaffar Iddi Maganga.

Pamoja na kumtangaza Pluijm, Maganga amesema watatangaza mchezaji mwingine mpya Jumatatu.

No comments:

Post a comment