Tuesday, 8 May 2018

Arsenal kumtangaza mrithi wa Wenger kabla ya kombe la Dunia

Klabu ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza inatarajia kumtangaza kocha wake mpya atakae rithi mikoba ya Arsene Wenger kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la Dunia mwezi ujao nchini Urusi.
 
Wenger raia wa Ufaransa amesaliwa na michezo miwili kabla ya kumaliza kwa ligi na kuondoka ndani ya klabu ya The Gunners baada ya ufalme wake wa miaka 22 kufikia kikomo.
Timu hiyo mpaka sasa haijatangaza muda maalumu wa ujio wa kocha wao mpya lakini kwa mujibu wa tovuti yake imeandika kuwa kabla ya michuano ya kombe la Dunia kuanza Juni 14 ya mwezi ujao basi itakuwa ishamtambulisha.
Kocha wazamani wa klabu ya Barcelona, Luis Enrique anahusishwa kujiunga na klabu hiyo akiwa sambamba na bosi wazamani wa Juventus, Massimiliano Allegri.
Wengine wanao husishwa na kupata dili la kuifundisha Arsenal ni pamoja na kiungo wake wazamani, Mikel Arteta na Patrick Vieira pia yumo kocha wa Monaco, Leonardo Jardim na mshindi mara tatu wa klabu bingwa barani Ulaya, Carlo Ancelotti.

No comments:

Post a Comment