Tuesday, 15 May 2018

Alikiba adai kuna wasanii wananunua views YouTube, ‘kwangu naona ni utoto’

Hitmaker wa ngoma ‘Seduce Me’, Alikiba amefunguka na kudai kuwa ni kweli kuna mchezo wa wasanii kununua views katika mtandao wa YouTube.

Kauli ya msanii huyo inakuja ikiwa ni siku moja imepita tangu wimbo wake mpya ‘Mvumo wa Radi’ kupata tatizo katika mtandao wa YouTube ambapo idadi ya views ilisimama na baadaye kushuka.
Katika mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema suala hilo lipo tena sana ila kwake ni kitu ambacho hakina maana.
“Tunajua kabisa kuna hizi bisness za kuweka maroboti katika hizi YouTube, watu wanajifanya wana views wengi na nini. Hivi vitu vipo, tena vipo!, vipo sana tu!, vipo tena sana boss!,” amesema.
“Eeeh, wananunua lakini kwa mimi binafsi naona ni utoto, mimi nafanya muziki wangu kwa ajili ya watu, kwanini nidanganye watu,” amesisitiza.
Katika hatua nyingine Alikiba amesema kile kilichotokea katika ngoma yake ‘Mvumo wa Radi’ halijaathiri muziki wake wala biashara yake yoyote ile.
“Haijaathiri chochote, watu wamepata walichokuwa wanataka na sio mimi nategemea pesa kutoka YouTube viwership, hapana!. Ninachotaka kwangu ni mashabiki wangu waridhike waelewe kabisa wana-deal na msanii wa aina gani,” amesema Alikiba.
Ngoma ya Alikiba, Mvumo wa Radi kwa sasa ina views zaidi Milioni 1.1 katika mtandao wa YouTube, ilitoka May11, 2018.

No comments:

Post a comment