Friday, 11 May 2018

Ali kiba afunguka ishu ya kutelekeza mtoto


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba amesema kuwa amesikia nakusoma kwenye magazeti malalamiko ya mzazi mwenzie Bi. Hadija ya kutelekeza mtoto wao lakini bado hajapata barua rasmi kutoka mahakamani.

Alikiba amesema mzazi mwenzie huyo aliinyanyasa sana familia yake kwani alikuwa hataki kabisa mtoto aishi kwa upande wa wazazi wake na alikuwa msumbufu.

“Niliiona kwenye gazeti, Hiyo ishu ipo ofcourse kwenye ustawi wa jamii, na yote mikasa ilitokana na jinsi yule mama alitunyanyasa sisi sote familia yetu jinsi ya kukaa na mtoto na kumuona. 

Kwa sababu mtoto anatamani kumuona baba yake basi labda unamwambia kwa leo Ijumaa mlete aje kukaa huku hadi Jumapili anarudi kwa ajili ya shule Jumatatu, lakini tukimchukua Ijumaa hiyo hiyo au Jumamosi anakuja kumchukua heti anam-miss, sikuwa namuelewa“amesema Alikiba kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

Hata hivyo, Alikiba amesema amefurahi kuitwa mahakamani kwani haelewi mpaka sasa lengo la mzazi mwenzie hususani kwenye malezi kwani kuna kipindi mtoto anafikia hadi hatua anataja jina lingine la baba yake kitu ambacho kilimfanya aache kutoa huduma kwa mtoto.

“Nilichokuwa nataka mimi ifike huko ilipofika (Mahakamani).. Kwa sababu haiwezekani kama kumuhudumia mimi nilikuwa namhudumia tena vizuri tu. mtoto nimemtoa kwenye shule aliyokuwa akisoma nimempeleka kwenye shule ya gharama zaidi ya mara tatu ya ile aliyokuwa akisoma. Sijaelewa lengo lake nini nini?,“amesema Alikiba.

Wiki iliyopita Alikiba alishtakiwa mahakamani na mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Hadija akidai kuwa msanii huyo ni mzazi mwenzie lakini hatoi huduma kwa mtoto.

No comments:

Post a comment