Friday, 13 April 2018

YANGA YAAHIRISHA MKUTANO WAKE NA WAANDISHI WA HABARI LEO

Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuahirisha Mkutano wake na Waandishi wa Habari uliopaswa kufanyika leo saa 7 mchana.

Yanga ilitangaza jana kuwa leo itaitisha kikao na Wanahabari ili kuzungumzia masuala mbambali yanayoihusu klabu hiyo.

Taarifa ya kuahirishwa kwa mkutano huo imeeleza kuwa ni sababu zisizozuilika, hivyo watapanga tarehe nyingine ya kikao hicho.

No comments:

Post a comment