Monday, 30 April 2018

Waziri Ummy amshukuru Alikiba

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amemshukuru msanii wa Muziki, Ali Kiba pamoja na mdogo wake, Abdu Kiba kwa kumualika katika sherehe yao baada ya kufunga ndoa.
Waziri Ummy amewatakia maisha mema yenye heri, furaha, baraka na maelewano pamoja na wake zao.
Asanteni sana @OfficialAliKiba na Abdu Kiba kwa kunialika kushiriki nanyi katika Siku yenu. Ninawatakia maisha ya ndoa yenye heri, furaha, baraka na maelewano pamoja na wake zenu Amina na Ruwayda. Hongereni sana🌺,“ ameandika Ummy leo April,30 kupitia mtandao wake wa Kijamii.

No comments:

Post a Comment