Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philipo Mpango amesema utaratibu wa kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ulikuwApo toka siku nyingi, lakini haukuwa wa kwenda mbele ya vyombo vya habari.

Dk Mpango ametoa kauli hiyo leo Aprili 13, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika utaratibu wa mawaziri kujibu hoja za CAG, leo ilikuwa zamu ya mawaziri wa habari na viwanda.

Amesema zamani kulikuwa na utaratibu wa Serikali kujibu kwa kuweka taarifa hizo bungeni, lakini wameona haifai kwa kuwa mwenzao CAG anaweka bungeni kisha kuita vyombo vya habari.

"Hakuna kukaa kimya, tunatumia sheria ya ukaguzi wa umma namba 418 (38) kifungu kidogo cha 3, Serikali inatakiwa kujibu na sasa tumeanza kujibu kwa kutumia njia anazotumia." amesema Dk Mpango.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: