Na Mahmoud Ahmad Dodoma
Serikali imewataka watumishi wa umma kujitathmini katika utendaji wao wa kuwahudumia wananchi wanyonge kwa matendo yao kama yanalingana na mwenendo wa mh. raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkta John Pombe Magufuli katika kuwahudumia wananchi wanyonge.

Kauli hiyo imetolewa jana na waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jaffo wakati akizindua mnara wa magufuli kwenye chuo cha serkali za Mitaa Hombolo ambapo amewataka kuhakikisha wanajitathmini katika matendo yao ya kila siku katika kuwahudumia wananchi.

Amesema kuwa wanafunzi wanaosoma hapo wanatakiwa kuanza kujitahmini kimatendo kama wana uwezo na moyo wa kuitumikia jamii kwani wajibu wao wa kwanza kujua wanaenda kushughulikia kero za jamii.

"Nawasihi vijana kuanza kujiangalia na kujitathini kiutendaji wao kama wanafanana matendo yao na mh.rais ili kuweza kuisaida jamii kwani wajibu wa msingi ni kufanyakazi kwa bidiii" alisisitiza Jaffo.

Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa chuo hicho Suleiman Ngware  wazo la kujenga mnara huo utakaoitwa (MAGUFULI SQUERE) Lilibuniwa na bodi ya chuo lieweka mbele maslahi mapana ya utendaji wa umma katika kutoa huduma bora bila kuangalia wala kubagua wananchi kwa hali zao.

Amesema kuwa sehemu hiyo ni sehemu ya kuanza kujitathmini kwa matendo yetu ya kila siku katika kuhudumia wananchi na wanafunzi watakao toka hapa wana wajibu wakuwa mabalozi wazuri katika utumishi wao ili taifa lifikie malengo kusudiwa.

Nae Mkuu wa Chuo hicho Dkta Mpamila Madale amesema kuwa kila tarehe kumi nane chuoni hapo watakaa eneo la mnara huo kuangalia suala zima la utendaji na kujitathmini kama wamefikia malengo katika utendaji wao wa kila siku.

Amesema kuwa mnara huo lengo lake ni kuwa chemu chemu ya utendaji unaofanana na mh.rais kufikia maengo ya kutoa watumishi wenye uzalendo na nchi yao ili kila mtanzania ajue wajibu wake kwa nchi yake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: