Watu saba akiwamo mwanamke mmoja wanashikiliwa na Polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii.

Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo amewaambia wanahabari leo Aprili 25 kuwa watu hao wamekamatwa kutokana na sababu za kuhamasisha maandamano Aprili 26 mwaka huu.

Ilembo amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakihamasishana kwa kutumia mitandao ya kijamii ikiwamo ya Telegram na WhatsApp.

Amesema watu hao wamekamatwa kupitia vitengo vya intelijensia baada ya kuwekewa mitego mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata.

Amesema miongoni mwa watuhumiwa hao baadhi yao wapo vyuo vikuu, mitaani na maeneo mengine.

Ilembo ameongeza kuwa watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote, huku wakiendelea kuwatafuta wengine kwa njia mbalimbali.

"Nasisitiza hakuna maandamano Aprili 26, atakayeandamana atavuna alichopanda kwa kuwa Serikali haijaribiwi," amesema Ilembo
Share To:

msumbanews

Post A Comment: