Mwanaharakati mmoja wa wanyama nchini Marekani ametekeleza tukio la kisasi la kuwashambulia kwa risasi wafanyakazi wanne wa mtandao wa YouTube baada ya malalamiko yake mengi aliyokuwa akiwatumia kushindwa kufanyiwa kazi.

Mwanaharakati Nasim Aghdam aliyetekeleza tukio hilo.

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Nasim Aghdam (39) mkazi wa California Jana Aprili 04, 2018 alitembelea Ofisi za Makao makuu ya YouTube mjini San Bruno na kufyatua risasi kwa kutumia bastola ambapo baada ya tukio hilo alijiua kwa kujipiga risasi mwenyewe.

Mtandao wa Washington Post umeeleza kuwa mwanamke huyo alitekeleza shambulizi hilo baada ya kutuma malalamiko yake kwa zaidi ya mara tano kuhusu mtandao huo kuwa unanyanyasa watumiaji wake na umekuwa na sera za kidikteta.

Baadhi ya malalamiko ya Nasim kuhusu malipo ya mtandao wa YouTube

Nasima alianza kuulalamikia mtandao wa YouTube kwa kuposti mabango kwenye mitandao miingine ya kijamii akitaka watu waususie mtandao huo kutokana na sera zake za kidikteta.

Mtandao wa YouTube umethibitisha taarifa hizo ambapo ulitangaza watu wanne kujeruhiwa vibaya lakini baadaye majeruhi watatu waliaga dunia.

Tayari Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa YouTube, Susan Wojcicki kupitia ukurasa wake wa Twitter ametoa pole kwa ndugu na jamaa waliyopatwa na tatizo hilo.

Hata hivyo, mpaka sasa hakuna taarifa yoyote mbaya kutoka kwa jeshi la polisi mjini California juu ya majeruhi hao wanne.

Rais wa Marekani, Donald Trump naye kupitia ukurasa wake wa Twitter ametoa pole kwa wafanyakazi wa mtandao wa YouTube.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: