Wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Deus Kaseke na Nizar Khalfan wamewekeza katika kilimo cha mazao ya mahindi na alizeti kwa lengo la kujiandaa pindi watakapostaafu  mchezo wa soka.

Wachezaji hao wa Singida United, wamesema kuwa wameamua kuingia katika kilimo kwani kinawasaidia kujiongezea kipato na kuwainua kiuchumi bila kutegemea mchezo huo.

Akizungumzia jana, Kaseke alisema kuwa ni vyema kuwaelimisha vijana kujiingiza katika kilimo ili waweze kujiwekea mazingira mazuri ya kiuchumi.

"Ninatumia mbolea za Yara katika shamba langu la ekari 16 ambapo nina lima zaidi mazao ya mahindi na imenisaidia kuyafanya mazao kupata muonekano tofauti na bora zaidi kulinganisha na wakulima wenzangu wa jirani. Kilimo kinalipa na haswa ukifuata kanuni za kilimo bora na chenye tija. Nawasihi vijana wenzangu muangalie fursa zilizopo katika kilimo," Alisema Kaseke.

Alifafanua kuwa wachezaji wengi wa mpira nchini, baada ya kustaafu wamekuwa wakiishi kwa taabu kwa kuwa hawajiwekei akiba hivyo yeye anajiandaa ili aweze kumudu maisha yake kwa kuwa na kipato endelevu.

Kapteni wa Singida United, Nizar alisema wamekuwa mabalozi wa Yara Tanzania kwa kuwa ni watumiaji wa mbolea hiyo mbali na kuwa wadhamini wakuu ila pia katika kilimo chake cha alizeti.
Alisema amekuwa akijihusisha na kilimo hicho kwa lengo la kujipatia kipato na kwamba upo uhitaji mkubwa wa mafuta ya alizeti.

"Mbolea hizi zimenisaidia katika kilimo changu kwani nimeweza kuongeza kipato kutokana na mavuno niliyopata nimetumia mbolea ya kupandia YaraMila Winner na kukuzia aina ya Sulfan ila msimu huu nimeweka YaraMila OTESHA ambayo ni mbolea mpya ya kampuni ya Yara. YaraMila Winner imesaidia kuvuna mazao bora na mengi kwa ajili ya kuuza sio tu kwa matumizi ya nyumbani. 

Vijana tunawaomba washiriki pamoja nasi katika kilimo hususani Kilimo cha alizeti ambacho uhitaji wake ni mkubwa. Kwa asilimia kubwa Tanzania bado inaagiza mafuta ya kula wakati tungeweza kuzalisha wenyewe na vijana ndio wenye nguvu kazi kubwa ya kufanikisha hilo," alisema Nizar.

Naye, Mstaafu serikalini, Erasto alisema mbolea za Yala  ni nzuri na zinaleta matokeo bora katika uzalishaji wa bidhaa bora za mashambani na wakulima wengi wameipokea.

"Hali ya mashamba ni nzuri kuliko mashamba yasiyotumia mbolea kwani sasa hivi shamba la ekari moja ninapata gunia 35 hadi 40 kulinganisha na hapo awali nilipokua nikivuna gunia 15 hadi 25 za mahindi," alisema
Share To:

msumbanews

Post A Comment: